Timu ya taifa ya Canada imefanikiwa kufuzu kucheza kombe la Dunia kwa mara ya kwanza ya ukame wa miaka 36 kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya Jamaica usiku wa kuamikia Jumatatu.
Canada hawajashiriki kwenye kombe Dunia tangu mwaka 1986 lakini kwa sasa wana kizazi cha dhahabu na ishara nzuri ilianzia walipoifunga Costa Rica 1-0 na walimaliza kazi jumapili hii kwa kuifunga Jamaica.
Walipanda hadi nafasi ya 33 mwezi uliopita wakati viwango vya dunia vilipotangazwa, nafasi ya juu zaidi kwa Canada kuwahi kutokea kwenye ngazi ya FIFA.
Canada wanahitaji kupata alama moja pekee ili waweze kuongoza kundi na mchezo wa mwisho wataumana na Panama ugenini mchezo utakaopigwa siku ya Jumatano.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.