Rudisheni Kombe na Medali Zote!

Ni baada ya kikao cha uongozi wa juu wa shirikisho la soka Afrika CAF, kukaa kwa dharura na kujadili matukio yaliyotokea katika fainali ya klabu bingwa Afrika kati ya Wydad Casablanca na Esperance kutokana na matukio yaliyojitokeza ndani ya mechi hiyo kuwa sio ya kimichezo kabisa.

Mechi hiyo ilikumbwa na migongano mingi iliyosababishwa na maamuzi mabovu ya muamuzi wa mchezo huo jambo ambalo lilizua tafrani kwa mashabiki ambao wakikuwa wanaona uhalisia wa mechi yenyewe na kile kinachoamuliwa na muamuzi kwamba kuna upande ambao unapendelewa zaidi.

Katika mechi ya awali Esperance wao ndiyo waliibuka washindi wa kombe hilo na kukabidhiwa vifaa vyote anavyotakiwa kukabidhiwa mshindi wa kombe popote duniani ikiwemo medali na kombe huku Wydad wakisusia kuendelea na mechi hiyo jambo ambalo liliwaumiza wao kutokana na maamuzi hayo ya hovyo.

Lakini kamati imegundua kwamba kulikuwa na mapungugu ya kiutendaji kutoka kwa muamuzi jambo lililowafanya washindani wa upande mwingine kugomea mechi yao. Kwa hali halisi walikuwa na haki ya kufanya hivyo baada ya mapungufu kuzidi sana uwanjani.

Rudisheni Kombe na Medali Zote!

Wydad, hadi sasa, wametwaa ubingwa wa ligi yao baada ya kuwa na msimu mzuri na wa pekee sana. Na kwa hali halisi hata kikosi chao kina ushindani wa aina yake pamoja na kwamba walisusia kuendelea kucheza mechi yao. Jeuri yao ya kutambua nafasi yao imewapa mafanikio hayo.

Itakuwa aibu kubwa sana kama klabu hiyo ya Tunisia watashindwa kutwaa ubingwa huo kwa awamu nyingine baada ya marudiano ya mechi hiyo. Fainali hiyo imefutiliwa mbali na itachezwa upya tarehe 30, Juni 2019 kwenye uwanja ambao kila klabu haitakuwa na mashabiki ndani ya uwanja huo nchini Afrika Kusini; uwanja huo wa ugenini utachangia mechi kuisha kwa utulivu.

Hilo linatokana na fujo za mara kwa mara ambazo zinatawala soka la Afrika kwenye mechi kubwa kama hizi. Aina hii ya mechi ndiyo huwa kikwazo kikubwa sana cha maendeleo ya soka barani Afrika kwa sababu hukatisha ile radha ya soka na kuonekana kila kitu kinaamuliwa tu kwa upangaji wa matokeo nje ya uwanja kati ya klabu husika na waamuzi ambao ndiyo huchezesha mechi hizo.

3 Komentara

    Duh majAnga

    Jibu

    Noma sana.

    Jibu

    Nishai waamuzi hakuna wenye vigezo

    Jibu

Acha ujumbe