Saka Kusaini Mkataba Mpya Karibuni

Winga wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Bukayo Saka anakaribia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.

Bukayo Saka amekua akifanya mazungumzo na klabu yake ya Arsenal kwa muda mrefu kwajili ya kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo, Taarifa zinaeleza makubaliano ya pande mbili yameshafikiwa baina ya mchezaji na klabu na winga huyo atasaini kandarasi mpya ya kuendelea kubaki kwenye viunga Emirates.SakaKlabu ya Arsenal imekua kwenye mpango wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu ndani ya timu hiyo, Huku tayari ikiwa imewaongezea mikataba wachezaji wake kama Gabriel Malgahes, Gabriel Martinelli, pamoja na Mohamed Elney ambaye wanatarajiwa kuwepo klabuni hapo kwa muda zaidi.

Kuongezewa mkataba wa Bukayo Saka ni jambo ambalo lilikua haliepukiki kutokana na namna mchezaji huyo ameboresha uwezo wake tangu ameanza kupata nafasi ndani ya timu hiyo, Kwani mchezaji huyo amekua akikua kila msimu ila msimu huu akionekana kuboresha zaidi uwezo wake.SakaBukayo Saka mpaka sasa anakua mchezaji ambaye anaongoza kwa kuhusika na mabao kwenye ligi kuu ya Uingereza ndani ya klabu yake ya Arsenal, Winga huyo mpaka sasa ameshahusika kwenye jumla ya mabao 22 kwani mpaka sasa amefunga mabao 12 na kupiga pasi 10 za mabao ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.