Bukayo Saka mchezaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza amefanikiwa kua mchezaji bora wa kiume wa mwaka nchini Uingereza baada ya kuchaguliwa na mashabiki wa nchi hiyo na kuwazidi wachezaji wengine ambao walikua wanashindana katika tuzo hiyo.

Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka kwa mtindo wa kupiga kura kwa mashabiki wa mpira wa taifa na kuchagua mchezaji bora wa taifa hilo,Saka amefanikiwa kuwashinda wachezaji wenzake wa timu hiyo Declan Rice pamoja na Harry Kane ambao walifanikiwa kuingia tatu bora na mchezaji huyo wa klabu ya Arsenal kuibuka mshindi wa tuzo hiyo.

sakaMchezaji huyo amekabidhiwa tuzo yake mapema leo kuelekea mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Italia utaopigwa usiku wa leo katika dimba la San Siro.

Saka amekua na msimu bora sana 2021/22 katika klabu yake ya Arsenal ambapo ameweza kubaki kwenye ubora huo mpaka wakati huu anafanikiwa kupata tuzo hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa