Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya Genk Mbwana Samatta ameipatia timu yake alama tatu za ushindi kwenye mchezo wao wa ligi ambapo walikuwa ni wageni kwenye mchezo huo walipocheza dhidi ya Union St. Gilloise.

 

Samatta Aipatia Genk Alama 3

Samatta na timu yake mpaka kufikia dakika ya 74 ubao ulikuwa ukisomeka ni moja kwa moja baada ya timu ya Union Gilloise kusawazisha bao hilo wakiwa katika viunga vyao vya nyumbani. Baada ya kuongezewa dakika, ndipo Mbwana akaifungia bao la uongozi Genk ambalo ndilo lililoipa timu yake alama tatu muhimu ambapo ilikuwa ni dakika ya 90+2.

Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars ana miaka 30 amejiunga na timu yake msimu huu kwa mkopo ambapo  alishawahi kucheza zamani kabla hajatimkia katika vilabu mbalimbali akiwa kwa mkopo pia  amejiunga na Genk kwa mkopo akitoka Royal Antwerp  ambapo amekuwa hapati sana muda wa kucheza.

 

Samatta Aipatia Genk Alama 3

Mshambuliaji huyo amecheza vilabu mbalimbali ikiwemo Aston Villa inayoshiriki Ligi kuu ya Uingereza ambapo pale hakuweza kudumu kwa muda mrefu kutokana na kukosa namba mara kwa mara klabuni pale, Lakini baada ya hapo akajiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, baada ya muda mfupi akatolewa kwa mkopo Royal Antwerp na sasa yupo Genk.

 

Genk katika mechi nane ambazo wamecheza katika ligi yao wameshinda mechi sita, wametoa sare moja, na wamepoteza mchezo mmoja, huku wakiwa katika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo ya Ubelgiji, na nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Royal Antwerp.

 

Samatta Aipatia Genk Alama 3

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa