FIFA: VAR kutumika Sambamba na 'Semi-Automated Offside Technology'

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limesema kuwa litaendelea kutumia teknolojia ya VAR sambamba na teknolijia mpya ya utambuzi wa mpira ya kuotea kwenye mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kuanza kwenye kipindi cha baridi nchini Qatar mwaka huu.

FIFA ilitambulisha teknolojia ya VAR kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini Urusi na kuwa mashindano ya kwanza kutumika duniani kabla ya kusambaa na kuanza kutumika kwenye ligi mbalimbali.

“Tunajua nini tunatarajia kutoka VAR kwa sasa  lakini kombe la dunia 2022 tutaona matumizi muengine ya teknolojia ya maamuzi ambayo ni ‘semi-automated offside technology’.

Mwezi july FIFA walitangaza kwamba ‘semi-automated offside technology’ ingetumika kwenye mashindano haya ya kombe dunia baada ya kufanyiwa majaribio kwenye mashindano ya ligi ya dunia ya vilabu.

FIFA wanadai kuwa visaidizi hivi vitawasaida waamuzi watakaochezesha michezo ya kombe la dunia kutoa maamuzi sahihi ya haraka kupunguza utata wa mipira ya kuotea.

Acha ujumbe