Klabu za Barcelona na Atletico Madrid zipo kwenye mzozo mkubwa wa kisheria kuhusu uhamisho wa nyota Antoine Griezmann ambaye anaichezea klabu ya Atletico Madrid kwa mkopo kwa msimu wa pili akitokea klabu ya Barcelona.

Klabu ya Barcelona iko tayari kuchukua hatua za kisheria ili kujaribu kuingilia mpango wa klabu ya Atletico Madrid wa kukwepa kulipa kiasi cha €40 million ambacho kipo kwenye kifungu cha makubalino ya uhamisho wa mkopo.

Griezmann, Griezmann Kuwapeleka Barcelona na Atletico Madrid Mahakamani, Meridianbet

Klabu ya Atletico Madrid itapaswa kuilipa Barcelona €40 million kwa ajiri ya huduma ya  Griezmann mwisho wa msimu  ikiwa tu atacheza asilimia 50% ya michezo yote, lakini pia atahesabiwa kama amecheza ikiwa atacheza kwa dakika 45 kwenye mchezo husika.

Atletico Madrid wanatumia mwanya wa kipengere hicho kwa kumcheza Griezmann dakika chache zaidi kwenye kila mchezo. Mpaka sasa Griezmann hajanikiwa kucheza dakika 45 za mchezo wowote kwenye msimu.

Barcelona wanaona klabu ya Atletico Madrid wanafanya uhuni na kujaribu kutumia mwanya wa kipengere hicho kukwepa kulipa pesa hizo ndio maana wamepanga kutafuta usaidizi wa kisheria.

Atletico Madrid watapaswa kuipa klabu ya barcelona €40 million ikiwa tu ndani ya misimu atacheza asilimia 50% ya michezo yote ambayo atakuwpo, ukiondoa majeruhi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa