Miliki wa klabu ya Chelsea Todd Boehly yuko mbioni kumshawishi mkurugenzi wa klabu ya PSG Luis Campos kujiunga na klabu hiyo ambayo kwa sasa iko kwenye maboresho ya kujenga timu baada ya kumfuta kazi Thomas Tuchel.

Todd Boehly inasemekana kuwa hana furaha na wala haridhishwi na mfumo wa klabu ya Chelsea kwa sasa na ameamua kutafuta mkurugenzi wa michezo mpya kwa ajiri kufanikisha sajiri kwenye dirisha la mwezi january baada ya dirisha hili la kiangazi klabu hiyo kusuasua sana kwenye usajiri.

Chelsea, Chelsea Yamuwinda Mkuregenzi wa Michezo wa PSG, Meridianbet

Luis Campos amejiunga na klabu ya PSG kwenye majira haya kiangazi lakini amefanya kazi kubwa ambayo imemvutia mmiliki huyo wa klabu ya chelsea baada ya kuhakikisha klabu ya PSG inapunguza wachezaji mizigo na kufanikisha sajiri mpya kwenye klabu hiyo.

Luis Campos kwa sasa anafanya kazi na vilabu viwili ambavyo ni PSG ya Ufaransa na Celta Vigo ya Hispania, lakini tatizo litakuja pale tu atakapo kubali kufanya kazi na Chelsea ambazo zote zinashiriki michuano ya ulaya na kuleta mgongano wa kimaslai kwa vilabu hivyo.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa