Christophe Galtier ametangazwa kuwa kocha mpya wa Paris Saint-Germain imethibitishwa na klabu hiyo ya Ligue 1 siku ya Jumanne.

Kocha huyo wa zamani wa Nice alikuwa akihusishwa kurithi majukumu ya kuifundisha PSG tangu mwezi uliyopita lakini sasa nirasmi ataihudumia klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Ilikuwa inajulikana mapema kwamba Pochettino ataachia majukumu hayo ambapo amekuwa meneja wa PSG kwa muda mwaka mmoja na miezi sita akifanikiwa kutwaa taji la Ligue 1 msimu uliyopita na mkataba wa sasa utaisha 2024.

Bosi huyo mpya alisema: “Nimefurahi kujiunga na Paris Saint-Germain, ningependa kumshukuru mwenyekiti Nasser Al-Khelaifi, mshauri wa soka Luis Campos na klabu kwa imani yao kwangu.

“Ninafahamu vyema majukumu yanayohusika kuifundisha timu hii ya ajabu, ambayo ni moja ya vikosi vya ushindani na kuvutia zaidi barani Ulaya.

“Nina furaha kufanya kazi na wachezaji hawa wote wenye vipaji pamoja na wafanyakazi wa ngazi ya juu hapa katika klabu. Tunatambua kila kitu ambacho Paris Saint-Germain inawakilisha katika soka ya Ufaransa na kimataifa.


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa