Baada ya Christiano Ronaldo kuomba kuondoka Manchester United basi kumekuwa na uvumi kwamba anaweza kujiunga na klabu ya Chelsea kutokana na tajiri mpya wa klabu kuvutiwa kufanya usajili wa mshambuliaji huyo wa Ureno.

Ronaldo Yupo Kwenye Mipango Tuchel?

Klabu ya Cheslea bado haijafanya usajili wowote mpaka sasa kwa sababu hiyo Boehly ameripotiwa kufanya mazungumzo na kocha wa The Blues Thomas Tuchel kuona kama kutakuwa na uwezekano wa nafasi ya Roanldo kwenye mipango yake.

Ingawa Tuchel anamipango ya kuboresha safu ya Ulinzi baada ya kuwapoteza mabeki wa timu hiyo ambao ni Antonio Rudiger na Andreas Christensen ambao wametimkia kwenye LaLiga.

Lakini walinzi waliyosalia Azpilicueta na Marcos Alonso bado hawajamalizana na Chelsea kama wataendelea kusalia klabuni hapo au wataondoka hivyo kusajili mabeki kulekea msimu unakuja italeta maana zaidi kwa Tuchel.

Tuchel anaumiza kichwa kuzipata saini za walinzi Jules Kounde na Mattijs de Ligt kwa hiyo akimalizana na suala la mabeki anaweza kuanza kufukiria kuwanasa washambuliaji.

Tajiri anatamani Ronaldo aende darajani lakini kocha vipaumbele vyake ni walinzi kwa sasa, acha tusubiri tuone picha linaendaje.


BASHIRI HAPA

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa