Eriksen kiungo wa klabu ya Manchester united anaamini klabu hiyo ipo kwenye njia nzuri na kusifu viungo wenzake kwenye timu hiyo.

Kiungo huyo ambaye alipata tatizo la moyo mwaka 2021 kwenye michuano ya ulaya kwa upande wa timu za taifa akilitumikia taifa lake la Denmark alifanikiwa kurudi uwanjani na kucheza klabu ya Brentford kabla ya kuibukia kwa mashetani wekundu majira haya ya joto.

Licha ya kupoteza mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Real sociedad kwenye michuano ya Europa league lakini timu hiyo inaonekana kuimarika kiuchezaji chini ya mwalimu mpya wa klabu hiyo Eric ten hag.

Akizungumza na tovuti ya klabu hiyo mdenishi huyo amesema”Viungo wa united walikua wanajitahidi kuzoea mbinu za mwalimu mpya.

eriksen

“Kila mtu ana ubora wa tofauti  ni juu ya mwalimu kuwaweka chini na kujua ni mchezaji atafaa mechi ipi mbinu ipi itafanya kazi alisema Eriksen”.

“Unamchukua Casemiro unamuingiza na anakuonesha namna yupo imara,Fred na Donny hawa wapo hapa kwa miaka sasa ni viungo wazuri”.

“Scott mctominay amefanya vizuri na utaliona hilo kupitia michezo aliyocheza hivi karibuni,kwenye michezo  ya kwanza tulikua tunajaribu kutafutana kidogo na kuangalia tulipo’.

“Nafikiri kwasasa tumeanza kupata muunganiko mzuri na kupata hisia nzuri juu ya sehemu tunayotakiwa kuwepo na kuzingatia maelekezo ya mwalimu kwasababu anajua tunapotakiwa kuwepo”.

Pia “kiungo huyo ameongeza unaposhinda mchezo inakusaidia kwani inatengeneza kujiamini na kusahau makosa madogo madogo uliyoyafanya huko nyuma na kukumbuka mazuri”.

Kiungo huyo anaamini kuna vitu vingi vya kuviimarisha lakini anaamini wapo kwenye njia nzuri.

“Msimu uliomalizika tulimaliza nafasi ya sita ila msimu huu tunanafasi ya kufanya vizuri zaidi kutokana na kikosi chetu kilivyo pamoja kuruhusiwa kubadili wachezaji watano itatuasaidia sana kufanya vizuri alisema kiungo huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa