Mlinda mlango wa klabu ya Cadiz, Jeremias Ledesma amepewa sifa baada ya kufanikisha kutoa msaada wa haraka kwa shabiki ambaye alipata matatizo ya moyo akiwa uwanjani akiangalia mchezo kati ya Cadiz na Barcelona siku ya Jumamosi
Mchezo ulisamishwa dakika ya 81 baada shabiki nyuma ya goli kuanguka huku Ledesma alikimbilia kisanduku cha huduma kifaa cha kushitua mapigo ya moyo kwa ajiri ya kusaidia zoezi la kumuokoa shabiki huyo.
Ledesma baada ya kupata vifaa hivi alirudi haraka sehemu ya tukio na kuwarushia watoa huduma za kwanza waliokuwa kwenye eneo la tukio. Baada ya video ya tukio hilo kuchachapishwa kwenye mitandao ya kijamii kuonesha tukio hilo ilisambazwa sana na wengi walitoa pongezi kwa kitendo hicho.
Shabiki huyo baada ya kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani aliwaishwa Hospitali na kupelekwa kwenye chumba cha waogonjwa mahututi, katika Hospitali ya Puerta del Mar ambako mpaka sasa bado anaendela kupatiwa huduma.
Mchezo uliendelea baada ya tukio hilo kudhibitiwa na mchezo kutamatika kwa klabu ya Barcelona kushinda goli 4-0