Twiga Stars timu ya taifa ya wanawake imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya tatu katika michuano ya Cosafa iliokua inaendelea nchini Afrika kusini.

Timu hiyo imefanikiwa kushinda mchezo wa nafasi ya tatu ulioikutanisha na timu ya taifa ya wanawake ya Namibia kwa mabao mawili kwa moja.

twiga starsChrister Bagera ndio aliwatanguliza Twiga stars dakika ya 12 tu ya mchezo akaipatia bao timu hiyo kabla ya Aisha Juma kuisawazishia Namibia kwa kujifunga,nahodha wa timu hiyo Emma Naris ndio aliepiga msumari wa mwisho na kuipa ushindi Twiga stars na kufanikiwa kumaliza kama mshindi wa tatu wa michuano hiyo.

Timu hiyo ya wanawake ndio walikua mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambapo walitwaa mwaka 2021 walipoifunga timu ya Malawi kwenye mchezo wa fainali kabla ya kuvuliwa taji hilo na timu ya wanawake ya Zambia kwenye mchezo wa nusu fainali baada ya kufungwa goli mbili kwa moja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa