Twiga Stars mabingwa watetezi wa michuano ya COSAFA wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja katika mchezo huo.

Timu hiyo ya wanawake ya Tanzania imetupwa nje ya michuano hiyo ambao walienda kama mabingwa watetezi wa michuano hiyo na kutupwa nje na timu ya wanawake ya Zambia ambao walionekana kua vizuri zaidi ya Twiga Stars katika mchezo huo.

twiga starsTwiga Stars walifanikiwa kuifunga timu ya wanawake ya Malawi katika mchezo wa Robo fainali ya michuano hiyo na kufanikiwa kufika hatua ya nusu fainali ambayo leo imechezwa leo na kuweza kutolewa.

Ni rasmi Twiga Stars wamelivua taji hili wealilokua wanalishikilia baada ya kulitwaa mwaka 2021 baada ya kuwafunga timu ya wanawake ya Malawi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa