Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal ya Uingereza, Sanchez alifanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi mnono wa 5-1 wa mabingwa wa Serie A, Inter Milan dhidi ya Sampdoria hapo jana.

Kabla ya mchezo kuanza, Inter Milan walipigiwa makofi na wachezaji wa Sampdoria kwa kufanikiwa kunyakua ubingwa wa Serie A. Na kilichofuata hapo ni mauaji makubwa kwa Sampdoria.

Inter Milan walitawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa sana, huku Sanchez akionekana kuwa na wakati mzuri zaidi katika mechi hiyo. Toka atimkie huko Italia Sanchez hakuwa na kipindi kizuri kama msimu huu ambapo amecheza mechi 28 tu na kuhusika katika magoli 13, akifunga 7 na kutoa asisti 6.

Kumaliza kwa msimu huu na kuonesha mchezo mzuri kunaweza kumhakikishia Sanchez nafasi nzuri ya kucheza katika kikosi cha kudumu cha Inter Milan msimu ujao.

Hakika mabingwa wa ligi zote wameamua kuonesha ubabe wao, kwani pia kule Ujerumani Bayern alimfunga Borussia Mongbagdach magoli 6 kwa 0. Siku ya leo Ac Milan watakuwa wageni wa Juventus pale Uwanja wa Juventus ambapo kila mmoja anatafuta tiketi ya kusalia top 4 ili kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

sanchez, Sanchez Atupia 2, Inter wakimfunga Sampdoria!, Meridianbet

SOMA ZAIDI

14 MAONI

  1. Kumaliza kwa msimu huu na kuonesha mchezo mzuri kunaweza kumhakikishia Sanchez nafasi nzuri ya kucheza katika kikosi cha kudumu cha Inter Milan msimu ujao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa