Mkurugenzi wa klabu ya Sassuolo, Giovanni Carnevali amethibitisha kuwa wamepokea ofa rasmi kutoka klabu ya EPL, Arsenal kwa ajili ya Manuel Locatelli.
Nyota huyu wa miaka 23 amekuwa na msimu bora uliopita klabuni hapo, akifanikiwa kuona nyavu mara nne na kutoa asisti tatu kwenye mechi 34 za Serie A alizocheza, wakati huo ameendelea kufanya vyema akiwa na timu yake ya taifa Italia kwenye michuano ya kimataifa ya Ulaya EURO 2020.

Taarifa za hivi karibuni zilibainisha kuwa klabu ya Arsenal tayari walikuwa wamewasilisha ofa yao ya awali kwa Sassuolo ya kuomba kumsajili nyota huyu wa Sassuolo, na Mikel Arteta alitajwa kuwa na nia ya dhati ya kumleta Locatelli kwa washika bunduki.
Kwa mujibu wa mkurugenzi Carnevali, ni kweli Arsenal wameshawasilisha ofa ya awali kwa ajili ya huduma ya staa huyo lakini wanapata ushindani mkubwa kutoka kwa Juventus.
“Arsenal wamewasilisha ofa ya awali ya kumsajili Locatelli. Wanafanya jitihada sana kumsajili Manuel na ni ofa muhimu. Tutaona itakuwajie. Juventus pia wanamuhitaji Locatelli na tuna uhusiano wa kipekee na wao. Mkutano mpya umeandaliwa na Juve”
Giovanni Carnevali
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

