Saudia Arabia Yaendelea Kuibomoa Ulaya

Klabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia zimeendelea kuleta balaa barani ulaya kwani zimeendelea kuzibomoa timu barani ulaya kwa kuchukua wachezaji wake.

Ligi ya Saudia Arabia imeendelea kufanya vurugu katika usajili kwa vilabu mbalimbali barani ulaya, Kwani mwanzo ilionekana kama wanasajili wachezaji ambao umri wao umesogea kidogo lakini kwasasa wamehamia hadi kwa vijana wadogo kabisa.saudia arabiaKlabu ya Al Ahli imefanikiwa kukamilisha dili la kiungo wa klabu ya Celta Vigo wa nchini Hispania Gabriel Viega mwenye umri wa miaka 21 hii ikiwa ni tishio kwa vilabu mbalimbali barani ulaya, kwani vilabu hivyo kutoka Uarabuni vimekua vikiweka ofa kubwa kwa wachezaji ambapo wamekua wakishindwa kukataa.

Wachezaji wa zamani na wasasa wameonesha kukerwa na kinachoendelea kwasasa katika soko la usajili na fujo za vilabu kutoa Uarabuni, Alianza Jamie Carragher kulaani na sasa Toni Kroos nae ameoneshwa kutofurahishwa na usajili hasa wa kijana Gabriel Viega.saudia arabiaVilabu kutoka Saudia Arabia vimefanya mapinduzi makubwa ya usajili kuanzia dirisha la mwezi Januari walipomchukua Cristiano Ronaldo, Lakini katika majira haya ya joto ndio wameonekana kua mwiba mchungu kwa vilabu mbalimbali barani ulaya.

Acha ujumbe