Kocha wa timunya taifa ya Argentina Lionel Scaloni amemzungumzia nahodha wa timu hiyo Lionel Messi na kusema milango iko wazi ya yeye kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Lionel Messi wiki kadhaa nyuma alifanikiwa kunyanyua taji la kombe la dunia nchini Qatar na maneno mengi yalizuka juu ya nahodha huyo kuendelea kutumikia timu hiyo ya taifa, Na kocha huyo amesema staa huyo bado anaweza kuitumikia timu hiyo.scaloniNahodha Lionel Messi ambaye amefanikiwa kushinda kila taji ambalo amewahi kushindania katika mpira wa miguu, Na kumpatia taji staa huyo ambaye amekua akilipigania kwa muda mrefu huku ikimchukua michuano mitano mpaka kufanikiwa kubeba taji hilo.

Kocha Lionel Scaloni anaona Messi anaweza kuitumikia timu hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia ijayo nchini Marekani na Mexico. Kocha huyo anasema suala la Messi kuendelea kuitumikia timu hiyo itategemea na Messi mwenyewe kuhitaji kuendelea kuitumikia timu hiyo.scaloniKocha Scaloni amesema kwasasa ana furaha kuendelea kuitumikia timu ya taifa ya Argentina, Kocha huyo amefanikiwa kua kocha watatu kubeba taji la kombe la dunia pamoja na Copa America baada ya Carlos Alberto Perreira na Mario Zagallo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa