Kikosi cha Simba SC leo Ijumaa Desemba 24, kitashuka katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kwa ajili ya kupambania alama tatu muhimu dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Wachezaji 24 wa Simba SC wamesafiri wapo katika afya njema na walifanya mazoezi jana jioni kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa leo utakao pigwa majira ya saa kumi jioni.
Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na kukosa muda wa kujiandaa baada ya wachezaji wengi kuugua siku chache zilizopita na kushindwa kufanya mazoezi ya pamoja.
Pablo ameongeza KMC ni timu nzuri na inacheza kwa ushiriakiano mkubwa uwanjani kuanzia katika ulinzi, viungo hadi washambuliaji hivyo tutaingia kwa tahadhari na kuwaheshimu.
“Mechi itakuwa ngumu KMC ni timu nzuri, hatujapata muda mrefu wa kujiandaa kuelekea mchezo huu lakini Simba ni kubwa hivyo tutajipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Pablo.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


