Tetesi zinasema, Sevilla wamejiunga na Barcelona katika kinyang’anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, Manchester United.
Tetesi zinasema, AC Milan wanamatumaini ya kumsajili winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 28.
Tetesi zinasema, Liverpool wanapania kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 19.

Newcastle United wamewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ijapokuwa klabu hiyo ya Uhispania inajaribu kurefusha mkataba wake.
Kiungo wa kimataifa wa Uingereza na Arsenal, Eddie Nketiah, 22, anataka kuondoka kwa ajili ya kutaka kucheza katika kikosi cha kwanza licha ya The Gunners kutaka kuongeza mkataba wake utakaokamilika msimu ujao wa joto.
Juventus wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 26, na mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32.
Meneja wa Tottenham Antonio Conte ameamua kusalia na winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, katika klabu hiyo licha ya vilabu vingine kumtaka.
Tetesi zinasema, Chelsea wana nia ya kumnunua beki wa Barcelona na Marekani Sergino Dest, 21.

Tottenham kwa sasa wanaongoza katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie. Timu hiyo ya kaskazini mwa London italazimika kupambana na Paris St-Germain, ambao pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Ralf Rangnick anajiandaa kuwasiliana na klabu yake ya zamani ya RB Leipzig kumnunua kiungo wa kati wa Mali Amadou Haidara, 23, huku akitafuta mbadala wa Nemanja Matic, 33, raia wa Serbia, Manchester United.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


