Formula 1, timu ya Mercedes imekuwa timu ya kwanza kutambulisha gari yao mpya watakayoitumia kwenye msimu wa 2022 huku wakitoa video fupi wakionyesha majaribio waliyokuwa wakiyafanya leo siku alhamisi.
Video iliyotolewa leo inawonyesha wafanyakazi wakiwa kiwandani wanatazama tukio hilo huku boss wa timu ya Mercedes Toto Wolff akitao maelezo kuhusu maendeleo mubashara kupitia akaunti ya Mercedes.

Utambulisho huo umekuja ndani ya wiki mbili tu baada ya fainali ya Formula 1 2021 kuisha jijini Abu Dhabi baada ya mbio hizo kuisha kwa utata, muundo huo mpya wa W13 unatarajiwa kufanyiwa majaribio mwezi Februari tarehe 23 mpaka 25 jijini Barcelona nchini Hispania, huku kukitarajiwa timu nyingine kutambalisha gari zao.
Picha zilizotolewa leo hazikutoa maelezo kamili kuhusu muundo mpya wa Mercedes ambao watatumia Lewis Hamilton na George Russell kwenye mashindano 2022 ya Formula 1.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


