Simeone: PSG Wanatumia Mamilioni, Atletico Inajitahidi

Diego Simeone, kocha wa Atletico Madrid, ameangazia tofauti kubwa ya kifedha kati ya timu yake na Paris Saint-Germain baada ya kichapo cha 4-0 katika mechi yao ya ufunguzi wa Kombe la Dunia la Vilabu.

Simeone: PSG Wanatumia Mamilioni, Atletico Inajitahidi

Atletico walishindwa kuonyesha makali yao, licha ya kuwa na nafasi chache za kuumiliki mchezo, ikiwa ni pamoja na kufunga bao ingawa lilikataliwa, na baada ya beki Clement Lenglet kuondolewa uwanjani, hali ikazidi kuwa mbaya na timu kulemewa kwa zaidi.

Ushindi huu wa PSG ulidhihirisha wazi utofauti wa ubora wa vikosi baina ya timu hizo mbili kwani kila mbinu waliyoitumia Atletico Madrid ili kuwadhibiti PSG iligonga mwamba na kugeuka kuwa shubiri kwa upande wao wenyewe.

Baada ya matokeo hayo Simeone alisema “Tulijaribu kwa kila namna, lakini haikuwezekana. PSG walikuwa bora zaidi, walitunyang’anya mpira na kuumiliki mchezo mara kwa mara.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Simeone: PSG Wanatumia Mamilioni, Atletico Inajitahidi

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 pia alitaja nguvu za kifedha za PSG, akisema: “Wakati Luis Enrique alipohitaji kuletewa winga wa kushoto, PSG walitumia €70 milioni Januari kumnunua mchezaji huyo (Khvicha Kvaratskhelia).”

Hii inaonyesha jinsi gani timu kama PSG inavyoweza kuimarisha kikosi chao kwa urahisi ikilinganishwa na timu kama Atletico.

Akizungumzia maamuzi ya mwamuzi, Simeone alikataa kuzungumzia suala hilo, akisema: “Baada ya miaka 14, nimechoka kuzungumza kuhusu waamuzi. Basi, nimechoshwa. Tofauti ya magoli ilikuwa ngumu, lakini sasa tunazingatia mechi ya tarehe 19. Mashindano bado yapo mbele yetu.”

Simeone: PSG Wanatumia Mamilioni, Atletico Inajitahidi

Kauli hizi zinaonyesha azma ya Simeone ya kusonga mbele licha ya changamoto, huku akionyesha tofauti ya rasilimali kati ya Atletico Madrid na vilabu vyenye uwezo wa kifedha kama PSG.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.