Chelsea wameanza kampeni yao ya Kombe la Dunia la Vilabu kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ya ligi kuu Marekani, LAFC, mbele ya maelfu ya viti vilivyoachwa wazi kwenye Uwanja wa Mercedes-Benz huko Atlanta.

Mchezo huu ulivutia watazamaji 22,137 pekee katika uwanja wenye uwezo wa kubeba watu 71,000, hali iliyoonyesha changamoto ya mauzo ya tiketi katika toleo jipya la michuano hii ya FIFA.
Pedro Neto aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 34, kabla ya Enzo Fernandez aliyetokea benchi kufunga la pili dakika ya 79 na kumpa kocha Enzo Maresca ushindi wa kwanza katika mashindano haya.
Licha ya idadi ndogo ya watazamaji, Chelsea waliweza kuonyesha ubora wao dhidi ya LAFC, wakiweka msingi thabiti wa kufanikisha safari yao katika Kombe la Dunia la Vilabu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mechi hiyo ilianza saa tisa mchana kwa saa za Mashariki za Marekani siku ya Jumatatu sawa na saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Muda huo unaelezwa kupangwa ili kuwapa wepesi watu wa Ulaya wanaofuatilia michuano hiyo kupitia Luninga.
Chelsea waliwahi kucheza mbele ya watazamaji zaidi ya 70,000 kwenye uwanja huo huo wa Mercedes-Benz mnamo Julai 2023, walipocheza na Newcastle kwenye mchezo wa kirafiki wa maandalizi kuelekea kuanza kwa ligi kuu Uingereza msimu huo.

Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, alisema kuwa ukosefu wa watazamaji kwenye mchezo huo ulifanya iwe vigumu kwa timu yake kupata matokeo.
“Mazingira na hali ya uwanjani yalikuwa ya kushangaza kidogo. Uwanja ulikuwa karibu tupu wakati wa mchezo wetu.” alisema Maresca.

Kocha wa LAFC, Steve Cherundolo, pia aliulizwa kuhusu idadi ya watazamaji baada ya mechi. Alisema: “Nadhani inategemea kila mechi. Huko Rose Bowl mjini LA, kulikuwa na umati mkubwa wa watu kwa mechi ya PSG na Atletico Madrid. Labda LA wanapenda soka zaidi kuliko Atlanta, sijui, tutahukumu baada ya kumalizika.”

