Chelsea imewaacha Raheem Sterling, Joao Felix, Axel Disasi na Ben Chilwell kwenye Kikosi cha wachezaji 28 kilichoitwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu huku Manchester City wakimbwaga Jack Grealish na Kyle Walker.
Mshambuliaji wa Man City, Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 29, alitarajiwa kutochaguliwa kwenye kikosi kinachoitwa baada ya kua na msimu mbovu kwani alifanikiwa kuanza mechi saba tu za ligi msimu wa huu.
Kikosi cha Manchester City chenye wachezaji 27 hakikumjumuishi nahodha wake wa zamani Kyle Walker, ambaye nusu ya pili ya msimu uliopita alikuwa kwa mkopo huko AC Milan, lakini kimemjumuisha beki wa Uingereza John Stones, ambaye hakucheza mchezo wowote tangu Februari kutokana na majeraha la paja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kikosi cha Chelsea kimewaacha wachezaji wanne ambao waligharimu pauni milioni 179 kwa ada za usajili, ingawa wote walimaliza msimu wakiwa wamekopeshwa kwa timu nyingine.
Sterling aligharimu pauni milioni 50 alipowasili kutoka Manchester City mwaka 2022, lakini mshambuliaji huyo wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 30 alicheza msimu uliopita kwa mkopo Arsenal, akianza mechi 13 na kufunga bao moja pekee.
Felix alihamia Chelsea kwa pauni milioni 45 msimu uliopita kufunga mabao saba katika mechi 20 kabla ya mshambuliaji huyo wa Kireno mwenye umri wa miaka 25 kumaliza msimu kwa mkopo huko AC Milan.
Chelsea ililipa pauni milioni 38.5 kumsajili Axel Disasi kutoka Monaco mwaka 2023, na beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 alicheza mechi 17 msimu uliopita kabla ya kumaliza msimu kwa mkopo huko Aston Villa.
Chilwell alisajiliwa kwa pauni milioni 45 mwaka 2020, na baada ya kucheza mechi moja tu ya Chelsea msimu uliopita, beki huyo wa kushoto wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 28 alienda Crystal Palace kwa mkopo, huku akikosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo na fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City alikua benchi.
Golikipa wa Serbia, Djordje Petrovic, mwenye umri wa miaka 25, pia hatasafiri kwenda Marekani, baada ya kucheza msimu uliopita kwa mkopo huko Strasbourg.