Wacheza Tenisi Wa Kike Kulinda Viwango Vyao Wakijifungua

Chama cha tenisi cha wanawake Duniani, (WTA) kimetangaza sheria mpya ya kulinda nafasi ya kiwango cha ubora kwa wachezaji wa kike pale wanapoingia kwenye majukumu ya uzazi, kama vile kulea ujauzito ama kulea mtoto baada ya kujifungua.

Sheria hii inalenga kuwasaidia wacheza tenisi wa kike kuweka sawa masuala ya familia bila kuwa na presha ya kupoteza nafasi zao za viwango vya ubora. Sheria hiyo itawahusu wachezaji wote walio katika nafasi 750 za juu za viwango vya ubora duniani ambao watakaa nje ya ushindani kwa zaidi ya wiki 10.

Wacheza Tenisi Wa Kike Kulinda Viwango Vyao Wakijifungua

Bingwa wa US Open wa 2017, Sloane Stephens, hapo awali alitaka suala la mapumziko ya uzazi kwa wachezaji wa kike wa tenisi kutambuliwa na wachezaji hao kulindiwa nafasi zao za viwango vya ubora na baada ya maamuzi hayo kutoka amepongeza na kuuita uhamuzi huo kama wa kihistoria kwenye mchezo wa tenisi.

“Kwa mwanamke yeyote, mfumo wa maisha ya familia dhidi ya maisha ya kazi ni mgumu sana na unahitaji mazingatio ya kina,” alisema Stephens.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Wacheza Tenisi Wa Kike Kulinda Viwango Vyao Wakijifungua

“WTA sasa imeunda nafasi salama kwa wachezaji kuchunguza chaguzi zao na kufanya maamuzi bora kwao wenyewe. Hii ni ya kihistoria kweli na itawapa nguvu wachezaji, kuendelea na mchezo wanaoupenda bila kulazimika kutoa sadaka mifumo ya maisha ya familia zao.”

WTA pia imesema kuwa wachezaji watanufaika na likizo ya uzazi yenye malipo na ruzuku za taratibu za kuhifadhi uzazi kupitia mfuko wa uzazi wa WTA unaofadhiliwa na mfuko wa uwekezaji wa umma wa Saudi (PIF).

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.