Murray na Rafael Nadal wameonyesha utofauti juu ya mustakabali wa maisha yao mara baada ya wote kustaafu mchezo wa tenisi. Murray alistaafu baada ya Olimpiki ya Paris, huku Nadal akicheza mechi yake ya mwisho kwenye Kombe la Davis mwezi Novemba mwaka jana.

Wawili hao walikuwa sehemu ya wachezaji maarufu wa tenisi, pamoja na Roger Federer na Novak Djokovic, waliovutia kizazi cha mashabiki wa tenisi ya wanaume na kufahamika Zaidi kwa jina la βBig Fourβ. Murray amestaafu akiwa mshindi wa mataji matatu ya Grand Slam, mataji mawili ya Wimbledon, na medali mbili za dhahabu za Olimpiki.
Baada ya kustaafu Murray aliwashangaza mashabiki wengi baada ya kutangaza kujiunga kwenye timu ya wakufunzi ya Djokovic, ingawa ushirikiano wao ulimalizika mwezi Mei.
Akizungumza huko Queenβs Jumatatu, nyota huyo wa tenisi wa Uingereza alikiri kwamba, yeye matamanio yake ni tofauti na Nadal, kwani bado anatamani kuwa kwenye uwanja wa tenisi.
Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Ninatamani sana kuwa hapa,” Murray alisema. “Hii ni mara ya kwanza kutoshiriki katika michuano hii, lakini sasa nina maisha mapya na ninafurahia kuwa mbali na mchezo kidogo.”
Hata hivyo, mambo ni tofauti kwa Nadal ambaye ana mpango tena wa kujihusisha na mchezo wa tenisi. Nadal alistaafu akiwa na mataji 22 na hivi karibuni alikiri kwamba hajajihusisha na jambo lolote linalohusu kucheza tenisi tangu alipotangaza kustaafu.
“Sitaki tena kucheza wala kujihusisha na tenisi kwa sababu nahisi nilijitolea kila kitu kipindi sijastaafu,” Nadal aliiambia waandishi wa habari mwezi uliopita. βNimekuja bila kuwa na hamu wala hisia za kuingia uwanjani. Mwili wangu hauniruhusu kuwa kwenye uwanja. Hivyo ndivyo ilivyo. Nina amani.

“Nilifanya yote niliyoweza kama mchezaji, na sasa ninafurahia awamu hii mpya ya maisha yangu, japo hayatakuwa ya kusisimua kama maisha wakati nikiwa mchezaji, kwa sababu adrenalini inayotolewa na michezo, nadhani haiwezekani kuipata katika mambo mengine maishani. Lakini hiyo haimaanishi kwamba sitokua na furaha.”
Alipoulizwa ikiwa amecheza tenisi tangu astaafu, Nadal alikiri: “Bado sijagusa raketi tangu nistaafu. Hivyo ni miezi sita bila kuwa kwenye uwanja wa tenisi. Lakini pengine naweza kurejea.β
“Nitarejea wakati fulani, kwa sababu inawezekana nikashiriki kwenye michezo ya maonyesho au kitu kama hicho.”


