Mara baada ya ligi ya EPL kukubali kufanya mabadiliko ya dharula katika upande wa ‘Subs’, moja kati ya watu walioipokea kwa furaha hatua hiyo ni kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer.
Sheria hiyo mpya ambayo imewekwa ili kumaliza msimu huu wa ligi, sio endelevu na imewekwa kama moja ya hatua zilizochukuliwa baada ya kuibuka kwa janga la Covid-19.
Ole Gunnar Solskjaer anaamini kuwa wachezaji watarudi viwanjani wakiwa hawana utimamu wa mwili wa kutosha kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu!
United watarejea uwanjani kwa mara ya kwanza kuwakabili Tottenham Hotspurs kabla hawajaumana na wabishi Sheffield United. United pia wana kibarua kizito katika mechi ya robo fainali ya mashindano ya FA dhidi ya Norwich.
Kitakua ni kipindi kigumu kwa Solskjaer na vijana wake wakipambana kufa na kupona ili kuifanya timu imalize katika nafasi za juu za msimamo! Marekebisho hayo ya sheria yanaonekana kuja wakati muafaka kabisa kwao.
“Ni msimu mfupi, tuna mechi tisa tu (za ligi kuu)! Lengo ni kupata alama nyingi kadri tuwezavyo!”
“Ninazingatia kila mechi inayokuja mbele yangu, lakini pia kujenga kikosi upya. Tuna kikosi chenye vijana wenye vipaji vya hali ya juu. Paul (Pogba) na Marcus (Rashford) wamerejea kikosini, Eric (Bailly) alikua nje kwa muda mrefu zaidi, Scott (McTominay) nae pia”, Solskijaer.
Marcus Rashford na Paul Pogba walipata muda wa kutibiwa majeraha yaliyokuwa yakiwakabili katika likizo hii ya Corona.
Solskjaer anaamini wachezaji wa namna hiyo, waliotoka kuuguza majeraha hawatoweza kucheza mechi nzima hivyo ameipokea kwa furaha sheria hiyo mpya inayowaruhusu makocha kufanya mabadiliko hata mara tano katika mechi, badala ya mara tatu iliyozoeleka.


Asha mvugalo
Gud news
Hope mwaikuka
Axante kwa taarifa
Devotha
Ni fursa kwake aitumie vema
Rehema Dickson
Ni fursa kwake maana wamekaa nje kwa kipindi kirefu sana sasa iyo itakua nzuri kwake nakwa timu pia
Tahiya
Ni habari njema kwa benchi la ufundi
Neema hassan
Habari njema#meridianbettz
Adelta
Good news #meridianbet
Antony Luseno
Hili sio kwake tu bali nahisi klabu zote zitakuwa zimefurahi na hili swala
Ester mmakasa
Asante kwa makala yenye kueleweka.
JULIANA
Habari njema
Salma
Ni habari nzurii
Theckla
Ashukuru kwa hilo
winfrida
hili limekaa viziri sana, nilijua ni endelevu
Elika
Benchi la ufundi liko vizuri
Warda
Hii nzuri sana#Meridianbettz
felister
habari njema kwa klabu zote
Samiah
Liko vzr benchi la ufundi
isha
Atoe pongezi maana sio kwa kuchekelea huko
Sylvester
Kwa mechi hizi za mfululizo itasaidia Sana hii
Sadick
Sheria imekuja muda muafaka kwa timu nyingi#meridianbettz
David Pere
Ni mfumo mzuri Sana maana kila mchezaji anapta furusa ya kucheza
Khadija
tunashukuru kwa makala nzuli ##meridianbettz
Ernest
Ni jambo zuri sana ukiazingatia wachezaji wengi wametoka walikuwa hawana mazoezi ya kutosha baada ya mapumziko ya muda mrefu kutokana na Corona
Dorophina
Ni Jambo zuri zaidi
Gabriel
Solskjaer lazma afurahie coz mson huu ajasajil sana na ukiangalia hii n sheria kwa club zote
Caroline
Yote ni maisha
lombo
solskjaer wakt wake mwache achekelee2
Lydia Emmanuel Magoti
Sheria imekuja muda muhafaka kwatimu nyingi
Hamidu
Subs! Kila mchezaji atapata muda wakucheza.#meridianbettz
Frank Patrick
Atafurah na roho yake akikutana na watoto wanaoupiga mwingi
Magdalena
Habari njema sana
Aziza mushi
Habari njema .
Genia Sikaluzwe
Hii itasaidia timu kufanya vzr,ni habari mzr kwa timu husika
Mwajuma
Itakuwa poa sana kila mchezaji atapata nafasi yakuonyesha kipaji chake
Povel
Ni furksa kwa wachezaj na makocha kufany mabadilik yaliyokuwah sahh thnks meridian bet tz kwa update
mwakalosi
sasa asifurahie tunataka kuona faida za hizo sub atakazozifanya ili tumalize ndani ya nafasi nne za juu
Shafii
Makala nzuri
Theonestina
Habari nzuri Sana kwetu sisi mashabiki wa mpira
Hidaya
Asante meridianbet kwa habari
Amani
Sipati picha mashibiki wa man u tunavyo furahi unajua nini top four lazima
Evaluziga
Ni fulsa kwake maana wamekaa nje kwa kipindi kirefu
Mwanaidi
Ni habari nzuri kwa bench la ufundi
Neema juma
Hii ni taarifa nzuri. Kutokana na kusimama kwa miezi kadhaa itawafanya warudi uwanjani kwa kasi nzuri na watacheza vzr
Ester jackson
Mwaka ni wenu makocha mfanye vitu vya kufurahisha sasa
julieth boniface
Tatizo timu yake mbovu sana
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
christopher
Anachekelea nn huyu mzee, maan Man u hakuna sub, nje wote wabovu
Kenani
Anapenda Sana Sabu hyu mzee
Zeiyana
Asichekelee tu sub tunasubili tuone matokeo mazur uwanjani
Agness
Habari njema