Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amemwaga sifa kwa viungo wake wawili Declan Rice anayekipiga Arsenal na Kobbie Mainoo anayekipiga ndani ya Man United.
Kocha Southgate alianza na Declan Rice akisema amekua na kiwango bora sana ndani ya kikosi hicho, Huku akijaribu kugusia ubora wa kiungo huyo kua amekua na uwezo mkubwa akiwa na mpira na hata pale ambapo hana mpira bado amekua bora.Kiungo Declan Rice hapokei sifa bure kutoka kwa kocha wake bali kazi yake pia inaonekana uwanjani, Kwani kiungo huyo amekua mchezaji muhimu kwelikweli kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kama ilivyo kwa klabu yake ya Arsenal.
Kocha Gareth Southgate hakuacha kutoa sifa kwa kiungo kinda mwenye umri wa miaka 18 ambaye jana alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya taifa ya Uingereza Kobbie Mainoo, Ambapo kocha huyo alisema kwa namna alivyocheza na utulivu wake inaonesha dhahiri atakuja kua mchezaji wa aina gani.Kiungo Kobbie Mainoo alifanikiwa kucheza dakika zisizopungua 15 katika mchezo wa jana huku akifanikiwa kuonesha ubora mkubwa, Jambo ambalo limemfanya kocha wake kutoa maoni chanya juu yake na kuamini atakuja kufanya vizuri zaidi mbeleni.