Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate ameweka wazi sababu za kutomjumuisha beki wa klabu ya Arsenal kwenye kikosi chake ambacho amekiita leo kwajili ya michezo ya timu hiyo.
Kocha Southgate amesema wiki iliyopita walipokea simu kutoka kwa wawakilishi ndani ya klabu ya Arsenal na kumueleza kua beki Ben White hataki kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.Kocha huyo amesema ni kitendo cha aibu kwa beki huyo kukataa kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Kwani Ben White ni moja ya wachezaji ambao anawapenda na angependa kuwajumuisha kwenye timu yake.
Kocha huyo aliendelea kwa kusema alimchagua beki huyo na kwenda kwenye michuano ya Euro mwaka 2021, halikadhalika kombe la dunia la mwaka 2022 na kocha huyo akisisitiza aliongea na beki huyo baada ya michuano ya kombe la dunia Qatar na kusema ni wazi kuna hali ya kutokutaka kwa upande wa mchezaji.Taarifa mbalimbali ziliripoti mwaka 2022 kua baada ya beki Ben White kutimka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza, Sababu ilikua ni kutokua na maelewano baina ya mchezaji huyo na enchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha Gareth Southgate.