Manchester City, kwa mara nyingine tena, anaenda kukutana na Spurs huku mechi hiyo ikitegemewa tena kuamua nani atakuwa bingwa kwenye ligi msimu huu. City hawatakiwi kupoteza mechi yao ya leo kwa sababu ni kioo cha wao kujua kama kombe msimu huu litalala tena kwao au upande wa majirani zao.
Sio mechi rahisi kwa wawili hao kwani wanakumbuka maumivu ambayo wamesababishiwa na ndugu zao hao kwenye michuano la klabu bingwa na kwa hakika wanarudi uwanjani upya wakiwa na maumivu ya aina yake baada ya kutupwa nje na klabu hiyo wanayoenda kukutana nayo tena kwenye awamu ya pili.
Mechi hiyo pia inategemea kuwa na ushindani upya kutokana na uhitaji wa alama kati ya wawili hao maana Manchester City anahitaji alama kwa kila namna ili aweze kuendelea kupanda juu ya ligi hiyo akimuacha Liverpool ambaye anaonekana kuwa na kasi na ajabu kuuhitaji ubingwa msimu huu.

Lakini kwa upande wa pili Tottenham wanahitaji alama ili waweze kujisilibia nafasi ya wao kuendelea kusalia nafasi nne za juu za ligi yao. Akiwa na tofauti ya alama moja pekee na Arsenal na Chelsea ambao wanamfuata kwenye nafasi hiyo. Hivyo basi ili kujijengea imani zaidi anapaswa kuchukua alama tatu leo kwani kuzikosa maana yake ni kuwapa nafasi wengine wakiwemo Chelsea na United kupanda juu kuchukua nafasi hiyo.
Si rahisi kusema ligi hiyo inakwisha kwa sasa kwa sabahu ushindani uliopo inaonekana kama ndiyo mwanzo wa ligi yenyewe. Maana upinzani kwa wakati huu ndiyo unazidi kuchukua nafasi ya hali ya juu kwa sababu katika klabu sita zilizo juu ya ligi hiyo kila mmoja anajitahidi kumuombea njaa mwenzake ili yeye apate nafasi ya kufanya vizuri.
Manchester City anatakiwa kukaza zaidi kwenye mechi zake ili aweze kupata nafasi ya kukaa kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa. Anatakiwa kushinda mechi zake zote zinazomkabili na kwa maana hiyo hatakiwi kabisa kuharibu upatikanaji wake wa matokeo huku akikabiliwa na mechi ngumu mbili ikiwemo kati ya United na hii ya leo ya Spurs.
Wakati pia wale wanne wanaopiganiana nafasi mbili zilizosalia kuweka timu nne za juu yaani Arsenal, Chelsea, Spurs na United wanapaswa kupigana kwa hali na mali ili kuchukua nafasi hizo. Japo United anakutana na ugumu kwenye ratiba yake kutokana na kuwa na mechi ngumu kati yake na Chelsea na ile ya kiporo kati yake na Manchester City.
Kinachosubiriwa na wengi kwenye mechi ya leo ni kwamba Manchester atakubali kupokea tena kichapo kingine ikiwa ni muendelezo wa historia ya Spurs au kwa wakati huu atajitahidi kujirekebisha na kugeuza matokeo kwa kulipa kisasi kwa mbabe wake huyo japo sio rahisi kwa City kupoteza mechi zake zote mbili akiwa nyumbani.

