Kisichomfurahisha Ronaldo Juventus

Baada ya kichapo dhidi ya Ajax na kupoteza nafasi ya kuingia nusu fainali. Cristiano Ronaldo anaripotiwa kuwa hana furaha tena klabuni hapo. Unafikiri nini kisichomfurahisha Ronaldo Juventus?

Taarifa zimebemba sana kuhusu Ronaldo Juventus, Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya michezo, Mirror, Gazzetta dello Sport na La Repubblica, nyota huyu aliondoka na hasira baada kushindwa gemu ya robo fainali.

Vyanzo hivi vinataja kuwa hasira za Ronaldo anazielekeza kwa meneja Massimiliano Allegri kwa kushindwa kumpa nafasi ya kuanza Joao cancelo ambaye Ronaldo anaamini angalau angekuwa ameleta mabadiliko kwenye mchezo huo.

Wakati kukiwa na sintofahamu ya hatma ya meneja Allegri, kuna taarifa zinazomtaja Antonio Conte kurejea klabuni hapo.

Ronaldo anadai klabu ya Juve inahitaji maboresho zaidi kuendana na kasi ya soka la Ulaya, anaitaka klabu hiyo kuingiza damu changa kikosini.

Staa huyu ambaye ameshinda Ballon d’Or mara 5 anadaiwa kuwa hafurahii sana kikosi alichonacho akihitaji msimu wa usajili utumiwe vyema kuwanasa watu sahihi, wakati huko staa kama Paulo Dyabala yuko mbioni kusepa kukamilisha dili la Joao Felix.

Mastaa wanaotajwa kuwa tageti ya klabu hii ya Serie A ni ‘mfalme wa misri’ kutoka Liverpool Mo Salah, Federico Chiesa wa Fiorentina na Tanguy Ndombel wa Lyon. Hata hivyo, bado wanapata upinzani kutoka kwa baadhi ya vilabu.

2 Komentara

    Nampenda sana Ronaldo

    Jibu

    Ronaldo anajua

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.