Kiungo wa klabu ya Liverpool ambaye anaitumikia timu ya taifa ya Hungury Dominik Szoboszlai anawasha moto akiwa na timu yake ya taifa ambapo ameshafanikiwa kuiwezesha timu hiyo kufuzu michuano ya Euro 2024.

Dominik Szoboszlai mpaka sasa ameshafanikiwa kuhusika na mabao matano kwenye michezo mitatu ambayo ameingia uwanjani kuitumikia timu yake ya taifa ya Hungury.szoboszlaiKiungo huyo ambaye amejiunga na klabu ya Liverpool akitokea Rb Leipzig ya nchini Ujerumani amekua kwenye kiwango bora na timu yake ya taifa, Huku akishirikiana na wenzake kuhakikisha timu yake ya taifa inafuzu michuano ya Euro 2024 nchini Ujerumani.

Kiungo Szoboszlai ambaye pia ameanza vizuri kwenye klabu ya Liverpool timu ya taifa ya Hungury ilikua na mchezo leo dhidi ya Montenegro ambapo Montenegro wamepigwa mabao matatu kwa moja, Huku kiungo huyo akifunga mabao mawili katika mchezo mmoja.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa