Kocha wa klabu ya Manchester United Eric Ten Hag amewataka wachezaji vijana ndani ya kikosi cha Manchester United kujituma zaidi ili kuweza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Kikosi cha Manchester United kimesafiri kuelekea nchini Hispania kwajili ya kuweka kambi kujiandaa na kurejea na ligi kuu ya Uingereza na michuano mingine ambayo klabu hiyo inashiriki, Huku ikiambatana na wachezaji wake kadhaa wakubwa huku kundi kubwa likiwa vijana wadogo kutoka akademi ya klabu hiyo.ten hagWachezaji takribani 12 kutoka timu ya kwanza bado wamesalia kwenye michuano ya kombe la dunia wakiwakilisha mataifa yao, Hivo imemlazimu kocha huyo kusafiri na idadi kubwa ya vijana kutoka akademi ya Manchester United.

Ten Hag anafikiri huu ni wakati wa vijana hao kuonesha kile walichokua nacho kwasababu sio jambo jepesi kufanya mazoezi na timu kubwa, Hivo wanatakiwa kutumia fursa hii kuonesha ubora mkubwa labda wanaweza kutoa ushawishi wa kupata nafasi kwenye mechi zijazo za ligi na michuano mingine ndani ya klabu hiyo.ten hagKikosi cha mwalimu Ten Hag kitarejea kwenye michuano rasmi tarehe 21 mwezi Disemba kwenye michuano ya EFL Carabao Cup na siku sita baadae itacheza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Nottigham Forest.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa