Ronaldo Aipongeza Ureno kwa Ushindi wa Kihistoria

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameipongeza timu ya taifa ya Ureno kwa ushindi wa kihistoria kwenye hatua ya 16 bora kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi.

Timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Uswisi kwenye hatua ya 16  bora baada ya kuigaragaza kwa mabao sita kwa moja ukiwa ni ushindi wa kihistoria kwenye michuano hiyo baada ya kupata ushindi huo mkubwa.ronaldoMabao matatu ya Goncalo Ramos aliyechukua nafasi ya Ronaldo aliyeanzia nje Pepe Lima, Rafael Guerrero, pamoja na Rafael Leao huku goli la kufutia machozi l timu ya taifa ya Uswisi likifungwa na beki anayekipa katika klabu ya Manchester City Manuel Akanji.

Nahodha huyo ambaye alianzia nje katika ushindi huo mkubwa lakini hakusita kuonesha kufurahishwa na ushindi huo huku akiandika kwenye mitandao yake ya kijamii “Siku nzuri kwa Ureno, Kwa ushindi wa kihistoria kwenye michuano mikubwa zaidi ya soka duniani. Mchezo mzuri kwa timu iliyojaa vijana wenye vipaji, Hongera kwa timu yetu. Ndoto yetu yetu Ipo hai mpaka mwisho”ronaldoRonaldo alianzia nje kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza bila ya kua na majeraha yeyote lakini kwa bahati nzuri kijana aliyechukua nafasi yake  Goncalo Ramos amecheza vizuri sana na kua mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu.

Acha ujumbe