Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag ameeleza kua kiungo mpya wa klabu hiyo Mason Mount anapaswa kupambania nafasi yake klabuni hapo kwasasa ambapo amekua hapati nafasi mara kwa mara.

Kocha Ten Hag ameweka wazi baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kwanini mchezaji huyo hapati nafasi ya kutosha klabuni hapo akijibu ni kwasababu alipata majeraha na nafasi yake ikachukuliwa na wengine ambao wanafanya vizuri kwasasa.ten hagKocha huyo ameeleza kua ni wazi majeraha yaliharibu kila kitu kwa Mason Mount kwani alikua anaanza kukaa vizuri, Lakini ghafla alipata majeraha ambayo yamekua kikwazo kikubwa kwake hivo anapaswa kupambana kurejesha nafasi yake aliyokua nayo.

Kiungo Mason Mount ambaye amejiunga na Manchester United katika dirisha kubwa lililopita akitokea Chelsea, Lakini amekua akipitia kipindi kigumu kwasasa klabuni hapo kutokana na kuandamwa na majeraha.ten hagKocha Ten Hag anaamini Mason Mount anaweza kurejesha ubora wake ndani ya klabu hiyo, Huku kipindi hicho akiwa anapaswa kupambana sana ili kurejesha nafasi yake ambayo imepotea kwasasa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa