Tetesi zinasema Barcelona huenda ikamsajili mshambuliaji wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane, 28, au kiungo wa kati wa Uholanzi Gini Wijnaldum, 30, baada ya kipengee katika makubaliano yaliyowezesha Philippe Coutinho kwenda Nou Camp kumalizika.

Mgombea urais wa Barcelona Emili Rousaud anasema ikiwa atachaguliwa atasajili “wachezaji wawili wazuri, mmoja wao akiwa Neymar”, mshambuliaji wa Brazil, 28, ambaye aliweka rekodi ya dunia ya uhamisho kutoka Barca hadi Paris St Germain mwaka 2017.

Tetesi zinasema Manchester United bado haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele lakini itajitahidi kufikia makubaliano ya mkopo kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 23.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.
 

Mkurugenzi wa Borussia Dortmund Michael Zorc anaona mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland ataendelea kusalia katika klabu hiyo “kwa muda mrefu” licha ya mchezaji huyo, 20, kuhusishwa na kuhamia Real Madrid.

Tetesi zinasema Chelsea inamnyatia beki wa kati wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25.

Tetesi zinasema Tottenham iko tayari kumsajili winga wa Leicester Demarai Gray, 24, kwa uhamisho wa bila malipo Januari.

Liverpool huenda ikapata kima cha pauni milioni 30 dirisha la usajili litakapofunguliwa Januari kwa kumuuza kiungo wa kati wa Uswisi Xherdan Shaqiri, 29, na mshambuiaji wa Ubelgiji Divock Origi, 25.

Tetesi zinasema mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 21, anakaribia kukubali mkataba mpya na AC Milan.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Manchester United imetoa ofa mpya kwa mchezaji Timothy Fosu-Mensah,22, wa Uholanzi anayeweza kucheza nafasi kadhaa ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao.

Tetesi zinasema West Brom inamfuatilia kiungo wa kati wa Celtic raia wa Ufaransa Ntcham, 24.

Aston Villa huenda ikatenga kitita cha pesa Januari kwa ajili ya winga wa Werder Bremen raia wa Kosovo Milot Rashica, 24, ambaye pia amehusishwa na RB Leipzig, Bayer Leverkusen na Wolfsburg.

Mchezaji wa QPR Bright Osayi-Samuel ameambiwa aache kuwa na wasiwasi huku winga huyo mzaliwa wa Nigeria, 22, akihusishwa na Burnley, Celtic, Fulham, Leeds United na Leicester.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa