Tetesi zinasema wawakilishi wa kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu uhamisho wake wa mkopo kwenda Nice, lakini mazungumzo rasmi yakitarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Meneja wa Newcastle Steve Bruce anauungwaji mkono wa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley, licha ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wanaotaka afutwe kazi baada ya kushindwa na Sheffield United kati kati ya wiki.
Tottenham huenda ikafutilia mbali mkataba wa Danny Rose katika dirisha la uhamisho wa Januari, huku West Brom ikionesha azma ya kutaka kumnunua beki huyo aliye na umri wa miaka 30.

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 32, ameamua kuacha £7m alizotarajiwa kupokea kabla ya mwisho wa msimu huu ili afanikiwe kukatiza mkataba wake na kuondoka mwezi huu.
Tetesi zinasema mlinzi wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20, amefikia makubaliano ya kibinafsi na Barcelona, lakini uhamisho wake haujakaribia kukamilika.
Meneja wa Barcelona Ronald Koeman ana imani ya kuwasajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26 kwa mkopo msimu huu.
Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Folarin Balogun, 19, amekubali kujiunga na RB Leipzig.
Tetesi zinasema Liverpool wanajiandaa kumsajili mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23.

Kiungo wa kati wa zamani wa England Jack Wilshere, 29, amemvutia kocha wa Bournemouth Jason Tindall na huenda akapata mkataba wa muda mfupi na klabu hiyo.
Tetesi zinasema Meneja wa Tottenham Jose Mourinho anasisitiza kuwa kiungo wa kati wa England Harry Winks, 24, hatauzwa au kutolewa wa mkopo mwezi huu.
Beki wa Everton Jonjoe Kenny huenda akaondoka klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la Januari, na Burnley wameonesha azma ya kutaka kumnunua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.
MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5
Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!



Caroline
Asante kwa taarifa
Rahmal
Tetesi ziko poa
Magdalena
Mourinho naon anataka kutengeneza kikosi kipana
Ernest Kimeru
Mambo moto sanaaaa
Shakila mrope
🔥🔥🔥
Saupha mohamed
Mambo moto
Sadick
muda umefika kwa Jesse Lingard kuondoka MAN U
Issa
Saf
David Pere
Tottenham huenda ikafutilia mbali mkataba wa Danny Rose katika dirisha la uhamisho wa Januari, huku West Brom ikionesha azma ya kutaka kumnunua beki huyo aliye na umri wa miaka 30.
Lydia Emmanuel Magoti
Ziko poa
felister
🔥
Hopemwaikuka
Liver Ben anafaa
Dorophina
Nice update
Sania
Kumekucha
Sarah
Ziko freshi