Tetesi zinasema, Arsenal inafikiria kumtumia beki wa Uhispania, Hector Bellerin, 26, kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez , 23. Tottenham wanamfwatilia pia iwapo watamuuza Harry Kane msimu huu.
Tetesi zinasema, Aston Villa iko tayari kukubali dau la Manchester City la £100m kumnunua kiungo wa kati wa England Jack Grealish, 25.
Kikosi hicho cha mkufunzi Dean Smith pia kitawasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Norwich na England Todd Cantwell, 23, iwapo Grealish ataondoka Villa Park.

Chelsea inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Atalanta, Bayer Leverkusen na Borussia Dortmund kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na klabu ya St. Etienne Lucas Gourna-Douath, ambaye atakuwa na umri wa miaka 18 kufikia wiki ijayo.
Tetesi zinasema, Manchester United inajianda kumpatia Luke Shaw, 26, kandarasi mpya baada ya mchezaji huyo kuonesha mchezo mzuri akiichezea England katika michuano ya Euro 2020.
Juhudi za klabu ya Tottenham kutaka kumsajili beki wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 Cristian Romero kutoka Atalanta zimegonga mwamba baada ya awamu ya mwisho ya mazungumzo kati ya klabu hizo mbili kukamilika bila makubaliano.
Tetesi zinasema, Beki wa Manchester City John Stones, 27, anakaribia kupatiwa kandarasi mpya , lakini mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mpya winga wa England Raheem Sterling yamegonga mwamba.
Tetesi zinasema, Fenerbahce inafikiria kumsaini beki wa Portugal na Arsenal Cedric Soares, 29.
Tetesi zinasema, Crystal Palace inafikiria kumsaini winga wa Arsenal Reiss Nelson, 21, kwa mkopo.

Juventus inatatizika kuafikia dau la pauni milioni 34 la Sassuolo kumnunua mchezaji wa Italia mwenye umri wa miaka 23 Manuel Locatelli, huku Liverpool na Arsenal zikiwa tayari kumsajili kiungo huyo.
Tetesi zinasema, Everton na Arsenal zinamfwatilia mshambuliaji wa klabu ya Schalke Matthew Hoppe 23, ambaye anaichezea Marekani katika kombe la Gold Cup.
Tetesi zinasema, Fulham ipo katika mazungumzo na klabu ya Flamengo kuhusu makubaliano ya dau la £6.8m ili kumnunua mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 20 Rodrigo Muniz.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!



Sarah
Tetesi ziko bomba
Sania+mapua
Nimezielewa hizi tetesi