Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Real Madrid itaweka kipengele cha kumruhusu Vinicius Jr, 21 cha 1bn euro katika mkataba mpya mshambuliaji huyo Mbrazil mwishoni mwa msimu.

Hatua ya Newcastle United kumtangaza Eddie Howe kama kocha wao mpya inasuasua baada ya kushindwa kuafikiana na Jason Tindall ili awe msaidizi wa Howe.

Manchester United imemuweka kocha wa zamani wa RB Leipzig, Ralf Rangnick katika orodha yake ya watakaorithi mikoba ya Ole Gunner Solskjaer iwapo atatimuliwa na Mjerumani huyo anavutiwa na mpango wa kuchukua kazi hiyo Old Trafford.

 

Kiungo wa Real Sociedad na Hispania Mikel Merino, 25, ananyatiwa na Liverpool ili kuboresha kikosi chao huku dau la usajili la nyota wa kimataifa wa England anayechezea Borussia Dortmund Jude Bellingham, 18, likionekana kuwa kubwa kwa wekundu hao wa Anfield.

Tetesi zinasema, Meneja wa Everton Rafael Benitez amepuuzilia mbali kwamba klabu hiyo ya Goodison Park itamwaga mapesa ya usajili katika dirisha la mwezi Januari.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Andriy Shevchenko anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Genoa baada ya klabu hiyo ya Italia kumtimua Davide Ballardini.

Tetesi zinasema, Kocha wa zamani wa Sheffield United Chris Wilder amekubali kuchukua mikoba ya kuinoa Middlesbrough baada ya kuondoka kwa Neil Warnock klabuni hapo.

 

Witsel Nje ya Dimba kwa Msimu Wote.

Tetesi zinasema, Juventus huenda ikatupa ndoano zake kwa kiungo wa Borussia Dortmund na Ubelgiji Alex Witsel, 32, katika dirisha la usajili la Januari.

Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis amesema uamuzi uko kwa mshambuliaji wa Italia Lorenzo Insigne kama ataamua kusalia kwenye klabu hiyo ya Serie A ama la, huku mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ukielekea ukingoni mwishoni mwa msimu ujao.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.