Tetesi zinasema, Liverpool imefikia makubaliano ya sheria binafsi na mshambuliaji wa Benfica mwenye umri wa miaka 22, Muruguay Darwin Nunez.
Tetesi zinasema, Manchester United wanatafakari uhamisho wa kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Muingereza Alex Oxlade-Chamberlain, 28.
Middlesbrough wamezungumza na Southampton kuhusu mkataba wa mkopo kwa ajili ya mshambuliaji Muingereza Adam Armstrong, 25.

Klabu kubwa zaidi za Ulaya zinaamini kuwa Raheem Sterling, 27, yuko tayari kuondoka katika Manchester City msimu huu, huku Chelsea ikiwa ni miongoni mwa klabu zinazomuwania.
Barcelona wamekuwa katika mazungumzo kumuhusu mchezaji wa Manchester City Bernardo Silva, 27 lakini wanaweza tu kusajili kiungo huyo, iwapo watamuuza kiungo Mholanzi Frenkie de Jong, 25.
Katika mkutano na maafisa wa Barcelona, wakala wa Silva, Jorge Mendes pia alijadili kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa AC Milan Mreno Rafael Leao, 22, na kiungo wa kati Mreno Ruben Neves, 25.

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Manchester City, Mjerumani Ilkay Gundogan, 31 ambaye mkataba wake unaendelea hadi 2023, anatakiwa na Barcelona na Juventus.
Tetesi zinasema, Chelsea na Tottenham zimejiunga na Manchester City katika kumuwania beki wa kushoto wa Brighton, Marc Cucurella, 23.
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.

