Kocha wa timu ya Brentford Thomas Frank amesaini mkataba mpya na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza na kutangazwa leo ambapo mkataba huo utafika tamati 2025.
Kocha huyo mwenye miaka 48 amabaye awali alikuwa kocha msaidizi chini ya Dean Smith,ambaye alichukua hatamu ya kuinoa timu hiyo yenye makazi yake jijini London mwezi oktoba 2018.
Msimu uliopita aliweza kuingoza klabu hiyo kuipandisha kutoka kwenye Championship hadi kufanikiwa kucheza ligi kuu ya Uingereza msimu huu, na kwa sasa wanashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Frank alisambaza video kwenye akaunti ya klabu ya twitter akionesha furaha yake yake ulisema, “najisikia fahari kuendelea kwenye safari hii bira kabisa, tumetengeneza historia kubwa na Brentford, natarajia kufanya vizuri zaidi siku hadi siku kujaribu kutengeneza historia mpya na watu wote hapa klabuni.”
Pia aliongezea kuwa msaidizi wake Brian Riemer nae amesaini mkataba mpya.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA