Kuna wakati mvua inadondoka lakini kuna Wachezaji wapo vile vile, wanaibadili akili yao kuendana na pitch na mpira unaendelea kupigwa
Kuna wakati barafu linadondoka huko Ujerumani, hata kuona huenda ni tabu ila wachezaji wanabadilika kutokana na uwanja na yanapigwa mabao ya kideo
Kuna wakati pitch haikuruhusu kuwa huru lakini inakupa sababu ya kuibadili akili yao kuendana na uwanja, kwakuwa Hali ya hewa ni UNPREDICTABLE
Wakati Mashabiki wanalalama kuhusu pitch ya Manungu, wakati Watu wanasema mpira hautembei, wakati baadhi ya wachezaji wa Simba wanapata kigugumizi cha miguu lakini sio kwa CLATOUS CHAMA
Yes ndio sifa ya Top Professional yoyote, anabadilika kutokana na uwanja ulivyo, Chama alipoingia Kuna kitu alikabadili kuanzia style ya uchezaji na namna ya kumiliki mpira usiathiri uchezaji wake
Mali ilikuwa inanata mguuni kama sumaku, very close ball control na akidribble anahakikisha mpira kaufichia ndani, alijua pitch haimpi nafasi ya kujiuliza bali mguu na mpira uwe sambamba kisha macho yawe mbele kuziona nafasi

Hizi ndio pitch zetu Kusini mwa Jangwa la Sahara, Wachezaji wetu wametokea huko na wanazijua vyema sana, hivyo sababu zinaendelea kuwepo ila Vipaji halisi vitaendelea kuonekana
Kwa yule anaesema pitch mbovu, kwa yule anaesema Manungu haifai, basi hakumuona Clatous Chama, ilikuwa kama siku nyingine za kawaida ofisini kwake, akitekeleza majukumu yake ya siku zote
Kinachotupa thamani katika Maisha sio mafanikio bali kuwa na utofauti pale ambapo sababu zinatafutwa, inaitwa SOLUTION
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


