Mlinzi wa kulia wa timu ya Liverpool Trent Alexander-Arnold ameachwa kwenye kikosi ambacho kitamenyana na FC Porto leo kwenye michuano ya klabu bingwa.
Alexander-Arnold alicheza dakika zote 90 kwenye mchezo dhidi ya Brentford ambayo walitoka sare ya 3-3, Alexander alionekana akifanya mazoezi na timu siku ya jumatatu lakini hakuwepo katika kikosi kilichosafiri kwenda nchini Ureno kukipiga dhidi ya Porto.

Inasemekana kuwa kutokuwepo leo kwa ni sababu ya mechi iliyombele ambayo wanawakaribisha Manchester CIty katika uwanja wao wa nyumbani Anfield siku ya jumapili.
Nafasi ya Trent Alexander-Arnold inatarajiwa kuchuliwa na James Milner au kinda Neco Williams japo dakika zake ni zauangalizi, Milner ananafasi kubwa ya kuanza leo.
Wachezaji wanaotarajia kuanza kikosi cha kwanza ni:- Alisson, James Milner,
Joel Matip, Joe Gomez, Kostas Tsimikas, Fabinho, Jordan Henderson, Curtis Jones, Mohamed Salah, Roberto Firmino , Takumi Minamino.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


