Tulimtaka Chama sio Bwalya - Hersi

MJUMBE wa Kamati ya Usajili wa Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, amesema hawakuwa na mpango kabisa wa kumsajili kiungo mchezeshaji mpya Simba raia wa Zambia, Larry Bwalya huku akisisitiza yeye alimuulizia Clatous Chama kwa meneja wake.

Hivi karibuni kuliibuka tetesi za Yanga kuwepo kwenye mipango ya kumsajili Bwalya kabla ya siku chache Simba kuchukua maamuzi ya haraka kufanikisha saini ya nyota huyo.Kiungo huyo amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga hapo akitokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika huko.

Akizungumza jijini Dar jana, Hersi alisema kuwa meneja wa Chama ndiye anayemsimamia Bwalya ambaye yeye alifanya mawasiliano naye kumuuliza kama kuna uwezekano wa kumpata Chama.

“Meneja wa Chama ndiye huyo wa Bwalya, mimi nilichofanya kumuulizia Chama nikionyesha nia ya kumsajili, lakini sasa kilichotokea ni meneja huyo kuwapigia simu viongozi wa Simba kwa ajili ya kuwajaza.

“Meneja huyo aliwapigia simu Simba kwa kuwaambia kuwa, Yanga wameonyesha nia ya kumsajili Bwalya kwa lengo la kuwaongezea kasi viongozi hao ili kukamilisha dili hilo la usajili haraka.

“Huyo Bwalya hatukuwa katika mipango naye kabisa, Chama kweli lakini siyo huyo kiungo, nikuhakikishie kuwa Yanga tukihitaji jambo letu hivi hakuna wa kulizuia kama tulivyoamua kwa Mwamnyeto (Bakari) kumsajili.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

42 Komentara

    Hersi yupo sahihi yanga nia yao ilikuwa ni chama na sio mchezaji mwingine tatizo simba wanapata tabu sana kuambiwa kwamba yanga wanamtaka bwalya wakamuwahi wao kumbe sio tegemeo la yanga chama angesajiliwa na yanga ingekuwa poa sana

    Jibu

    mhhh yanga singe weza kuwapata wachezaji hao bhana

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Mh yanga mnatapatapa sana mnapesa ya kumnunua chama nyie#Meridianbettz

    Jibu

    yanga tukiamua jambo letu hakuna wa kutuzuia#Mwajumah

    Jibu

    Lakini sio mbaya.kikosi kipo vizuri.wasubiri Mambo mazuri kutoka yanga

    Jibu

    Maneno mengi ya nini leo ndio tutaanza kuona jambo la wananchi pale kwa Mkapa

    Jibu

    Tatizo yanga wanamaneno mengi

    Jibu

    Duh noma sana hiiii

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Maneno mengi yanini

    Jibu

    Chama niwasimba tuuu akuna chama watimu nyingine atabaki kuwa Simba sio krabu nyingine

    Jibu

    Ikiwa kweli alimuhitaji Chama nadhani alitakiwa kuongea na Simba ambayo Chama anachezea kwa sasa,tatizo timu zetu zimekuwa zikikurupuka na kuvamia mambo mwisho wa siku zinaishia kwenye migogoro inayoweza kuepukika#meridianbettz

    Jibu

    Yanga mpya naiona

    Jibu

    Roho ya simba fc ni chama kwa sasa sidhani kama wangemwachia

    Jibu

    Yanga hamna maajabu kila siku maneno nyie jamani

    Jibu

    He kumbe!

    Jibu

    Asante kwa kunijuza

    Jibu

    Aisee noma sana

    Jibu

    Yanga mbwembwe nying,tunataka vitendo!!!

    Jibu

    Chama yuko vizuri sana.

    Jibu

    Maneno ya mkosaji hayo

    Jibu

    Simba wasinge weza kumuuza pia yanga Awana ela ya kumnunua

    Jibu

    Yangaa badoo sijawakatia tamaa

    Jibu

    Yanga muwaache wafanye yao

    Jibu

    mambo ni moto na meridianbet

    Jibu

    Dakika 90 ndio zitaongea

    Jibu

    Yanga bado wanakikosi kizuri tu

    Jibu

    Yanga Anna kitu

    Jibu

    Yanga haina shuhul

    Jibu

    Hana jambo jipya

    Jibu

    Mambo meus hapa hakun maajabu

    Jibu

    Kumsajil mchezaji sio tatinzo tatizo lipo kwa makala wao na timu zetu zinawasiliano mazuri lakini hakuna kabisa hawawezi wakupe bati wakati nyumba yao yavuja huu utakuwa uzembe

    Jibu

    Chama akiwa Yanga ni raha tupu

    Jibu

    Hatuwezi kumwachia kabisa Chama

    Jibu

    yanga wapambane wawezavyo ila chama kumpata sio rahisi watafute tu mtu mwingine watuachie chama wetu sisi wana simba tena watulie kabla hatujawafokea

    Jibu

    Kumbe bwalya hakua kabisa kwenye mipango ya yanga.

    Jibu

    Ikiwa kweli alimuhitaji Chama nadhani alitakiwa kuongea na Simba ambayo Chama anachezea kwa sasa,tatizo timu zetu zimekuwa zikikurupuka na kuvamia mambo mwisho wa siku zinaishia kwenye migogoro inayoweza kuepukik

    Jibu

    Yanga wako vzur hawahitaji mchezaji yoyote kikosi Kiko vzur huyo chama tokea akutwe na irizi hana maajabu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.