Kiongozi mkuu wa michuano ya Olympics, Thomas Bach amesema kuwa mwaka 2021 ni uamuzi wao wa mwisho juu ya ni lini michuano hiyo itafanyika tena ikiwa ni baada ya michuano hiyo iliyopangwa kufanyikia Tokyo kusogezwa mbele.
Ameyasema hayo siku ya Alhamisi akikazia suala la kwamba haiwezekani michuano ile ikasogezwa mbele zaidi ya ilivyo sasa.
Wakati Bach akizungumza na BBC aliwaambia kuwa amekubaliana na maoni ya Japan kuwa gemu hizo zitatakiwa kusimama kwa muda kutokana na janga la Corona na itatakiwa kuendelea endapo ugonjwa usipopatiwa ufumbuzi hadi kufikia mwakani.
Mwezi Machi, michuano ya Tokyo 2020 Olympics iliahirishwa mpaka ifikapo Julai 23, 2021 wakati maambukizi ya ugonjwa wa Corona yakiwa yamepamba moto kwa sasa duniani na kupelekea michezo mingi kusimama kabisa.
“Ni sahihi kwamba ninaelewa hali ya Japan kwa sasa lakini huwezi kuacha hali hii ikaendelea milele,” rais huyo wa International Olympic Committee alisema.
“Huwezi kubadili michezo yote kwa mwaka mzima duniani kote kwa mashindano yote makubwa.
“Hauwezi kuwaweka katika sintofahamu wachezaji wote wanaohusika, hauwezi kuruhusu hali hii ikaendelea milele hasa katika michuano ya Olympic.”
Michuano ya Olympics haijawahi kufutwa ukiachana na nyakati zile za kutokea kwa vita za kidunia lakini Wajapan na viongozi wao wamesema kwamba kwa sasa hawana lengo la kuendelea kuahirisha zaidi michezo hiyo zaidi ya hapo mwakani.


frank patrick
ni swala la kumuomba MUNGU tu hali ikae sawa Olympic sio bora zaidi ya Uhai wa watu bhana
Theckla
Ni lazima wakubali Hali halisi ilivyo kwa sasa
Theonestina
Corona imeasili vitu vingi Sana duniani.mungu atunusuru kwakwer
Neema juma
Mmh asante kwa taarifa #meridianbet
Povel
Ni Jambo la kuwah nasubir tu mpka Hali itakapo kuwah sawa kwn ni janga la dunia
Lombo
gud newz asante
winfrida
kila kitu kitakaa sawa kusogezwa mbele sio mwisho
Kenani
Tuombe mungu mambo yakae sawa
Salma
Wakubaliane na hari ilivyo sasa
Tahiya
Tuombe Mungu na kuchukua taadhari hakika kila kitu kitakuwa sawa
Gabriel
Tnx 4 news# meridianBetTZ
Swai
Kikubwaa ni kumuombaa Mungu na kuchukuwa tahadhari
Juliana
Uvumilivu nijambo zuri,maana kwa ugonjwa huu wa corona sio poa kabisa
Furahav
Habari nzuri
mwakalosi
sidhani kama wajapan wamefurahi maana walikuwa walazimisha sana michezo iendelee
David pere
Safi Sana maana kila kitu kina nafasi yake kwenye maisha
Ester mmakasa
Ni sawa ni kuomba uzima tuu .
Genia Sikaluzwe
Ahsant sana meridianbet kwa habari njema
Hope mwaikuka
Hili gonjwa liishe tu
Emmy cleopa
Habari nzur
felister
ni kumuomba mungu tu ili gonjwa litokomee mana ni la balaa
Antony Luseno
Maamuzi mazuri yamefanywa na kamati hii
Antony Luseno
Maamuzi mazuri yamefanywa na kiongozi huyo
Carolyne
Ni katika kujilinda na covid19
Warda
Corona kajua kutuaribia mambo#Meridianbettz
Ernest
Ni uamuzi sahihi japokuwa unaweza kutenguliwa muda wowote.
aisha
ahsanteni meridianbet kwa habari motomoto
Khadija
Meridian mnanipa furaha kwa taarifa motomoto#meridianbettz
Devotha
Tumuombe Mungu uzima tufike salama hiyo 2021
Shafii
Habari njema
Issa
Olimpik ni michezo mizuri