Wengi tumekuwa tukimtupia lawama Ibrahimu Ajibu kushindwa kutambua thamani ya kipaji chake angalau aionje pepo ya soka la kulipwa huko ng’ambo.
Ni mwendawazimu tu atakidharau kipaji maridhawa alichonacho Ajibu ila akisema neno katika utunzaji wake , nia ya kufika mbali basi hapo anaweza kuwa ameianza safari ya kueleweka na wadau wote wa soka nchini.

Wakati jana nautazama mpira wa watani wa jadi hususani idara ya kiungo ya Simba SC iliyokuwa chini ya mkongwe Jonasi Mkude , nilitafakari mambo mengi sana . Moja ya tafakuri yangu ilikuwa kwa wale ambao wanaomnyooshea kidole Ajibu , wapo wapi au tangu huyu mwamba anaibuka na sasa anaianza safari yake ya magharibi ya soka hawajamuona?
Jonas Mkude naweza sema ni mmoja wa viungo hatari nchi hii ambao wanaijua vyema kazi ya kiungo mkabaji na variations zake zote. Ni miaka takribani 10 thamani ya kiungo huyu haijawahi kushuka wala kutetereka nchi hii.

Unaweza kukaa na kujiuliza nini kimempata classic player kama huyu kushindwa kuvuka mpaka wa nchi yetu kwenda ng’ambo kuongeza thamani ya soka lake .
Katika vikosi vyote vya jana kwa Simba na Yanga , Mkude ndio alikuwa mchezaji pekee ambaye amecheza mechi nyingi za watani wa jadi, hivyo alikuwa na uzoefu wa kutosha kabla ya Yondani kuingia kipindi cha pili ambaye ndio mchezaji anayeshikiria rekodi kwa sasa Tanzania kucheza mechi nyingi zaidi za watani wa jadi .

Mkude kumalizia soka lake nchini ni mwendelezo wa soka letu kwa ujumla kushindwa kuwatoa nje wachezaji wenye vipaji vizuri kwenda kuongeza thamani ya vipaji vyao.
Ni wakati sasa kwa wachezaji chipukizi pamoja na viongozi wao kuinua macho yao ili waweze kutazama mbali zaidi kuliko kuridhika na malisho haya ya nyumbani. Wengi tulimshuhudia Feisal jana akiwa bora katikati ya kikosi kibovu cha Yanga kilichokubali kichapo cha 4-1 kutoka kwa Simba.
Feisal ni hazina kwa taifa endapo katika umri huu mdogo atapata njia sahihi ya kwenda mbali kisoka . Licha ya kufika EPL , Samatta amekaririwa akisema anatamani angefika katika ligi hiyo kubwa duniani akiwa na umri mdogo . Hii inaonesha ni vyema kuyaandaa mafanikio yako angali bado una nguvu na damu inachemka.

Kuna ofa kibao sana unzaofaidi ikiwa unabashiri na Meridianbet. Jiunge sasa kufurahia ofa zetu.
Bonyeza HAPA Kujiunga.


Tatu
Ukizungumzia kikosi cha simba ukosi kumuonge4a jonas mkude ni kiungo machachari tatizo nyota kinachomfanya akose kucheza clabu za nja
Neema juma
Mmh asanteni kwa taarifaa
Ernest
Hapa huwa napata shida kujua kama ni wachexzaji wenyewe ndio hawataki kuvuka mipaka au kuna kitu nyuma ya pazia
Magdalena
Uenda wakawa wanatamani kutoka nje lakini hawajapata connection yoyote ya kuwatoa nje
Dorophina
Tnx meridian kwa update za kimichezo
Flomena
Huenda wachezaji wenyew ndio hawataki kuvuka boda
Franky
Good news
caroline
jonasi mkude ni moja wa kiungo mahiri sana
Ester jackson
Asante
Omary lukumbi
Asante kwa taarifa
Genia Sikaluzwe
Ahsant meridian kwa taarifa
Salma
Kweli kabsa vizuri kundaa matarajio yako ya mbele bado una umri mdogo
Lydia Emmanuel Magoti
Mkude nikiungo mzuri Sana mpambanaji Sana yani atakama anakasolo zake zaujeuli nikawaida sisi binadamu atuja kamilika lakini mkude yeye binafsi yake anajua kulitumikia soka na hanajua nn anakifanya mpambanaji huyo ajawai kushuka kisoka kiungo mshambuliaji bek huyo anajua
Issa
Wachezaji wengi hawana mitazamo ya mbali wanaona kufika simba ama yanga ndio wamemaliza
felister
mchezaji mwenyewe mawazo ayo hana akichezea yanga au Simba anaona kashafika
Furahav
Tatizo wachezaji wetu wanacheza na majini mfukoni,waonekana wazuri kumbe wanamajini mfukoni,wakitoka nje wanakuwa hakuna kitu.
Angelina
Naona tatizo connection
isha
Makala safi
Njiku
Wachezaji wetu wanataka kucheza simba au yanga ndio mitazamo yao
Fatuma kasomo
Asante kwa taarifa
MnonganeJR
Ajibu talent player#meridianbettz
David Pere
Lakini bado hajitambui Ndio maana anabakia kuwa mchezaji wa ridhaa tu mpaka mwisho wa soka lake
Evaluziga
Asanten kwa taarifa
Zeiyana
Feisali bado kijana mdogo sana lakini hanaonesha hana uwezo mkubwa sana lakini hajapata timu ya kuichezea ushauri wangu hasikate tamaa kwani kufanikiwa kunatakiwa kujitoa sana..!big up sana dogo kazi yako inaonekana
Amiri Kayera
Kwer kbx
Hope mwaikuka
Kila ktu kina mda wake
Rehema
Bonge la makala
Gabriel
Kawaida sana
Saupha mohamed
Good news
Shafii
Makala iko vizuri.
sabrina
Asante kwa taarifa
Povel tz
Habar njema
JULIANA
Kweli mnatupa ufafanuzi akinifu kabisa,ndani Ajibu pembeni Mkude
Samiah
Nihabari njema
Mwanahamisi
Asante kwa taarifa
Elika
Makala nzuri sana hii
farida ahmadi
Habari nzuri Sana
devotha
asante kwa makala
Theonestina
Asanteni meridianbet kwa makala nzuri