Ukimtaka Luis Miquissone Ujipange - Simba

Nyota wa Simba, Luis Miquissone mbali na TP Mazembe pamoja na Al Ahly kutajwa kuwania saini yake pia inaelezwa kuwa CD Belouizdad ya Algeria, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kwamba dau la mchezaji huyo sio la kitoto hivyo timu ambayo inahitaji kupata saini yake lazima ijipange.

“Unajua wengi wanauliza kuhusu Luis, yule ni aina ya wachezaji wa kipekee na wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja hilo lipo wazi.”

“Sasa tunajua kwamba kupitia mashindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa anachokifanya yeye pamoja na wachezaji wengine mawakala wanahitaji huduma yake sasa kumpata lazima zijipange kwa kweli.”

“Naweka wazi kabisa dau la kumpata Luis kwa sasa ofa yake ya mwisho haiwezi kuwa chini ya Euro milioni moja hiyo ni ofa ya mwisho kabisa kwa mchezaji wetu.”

“Dunia ya sasa inatumia Euro zaidi hivyo ofa yake haiwezi kuwa chini ya hiyo, nasema hivi hicho ni kiwango cha chini, kama Bwalya (Walter) kauzwa kwa dola milioni moja Al Ahly kwa nini Luis auzwe kwa chini ya kiwango hicho?”

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuwaniwa na timu nyingi kutokana na uwezo wake ndani ya uwanjani mbele ya Al Ahly wakati Simba ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa alitupia bao bora ambalo limezidi kumfanya awe gumzo.

Ikiwa kundi A inaongoza kundi na pointi zake ni sita, mechi zake mbili imeshinda zote ya kwanza ilikuwa ugenini dhidi ya AS Vita na ya pili mbele ya Al Ahly zote ilishinda bao mojamoja.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

7 Komentara

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Simba wakiamua Jambo wanafanya tu

    Jibu

    Kwa ilo goli moja

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Imeeleweka hii

    Jibu

    Hiko sawa hii

    Jibu

    Wasubilie kwanza tuchukue club bigwa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.