UWANJA wa Majaliwa sasa utatumika kwa mechi za nyumbani kwa Klabu ya Namungo baada ya kufanyiwa marekebisho ambayo yalichukua muda mrefu, tangu katikati ya msimu uliopita.

Wakati wa maboresho hayo, Namungo FC ilikuwa inatumia Uwanja wa Ilulu uliopo Lindi na uwanja wa Ilulu ulipofungiwa pia ili ufanyiwe maboresho walikuwa wanatumia Uwanja wa Mkapa na Uhuru kwa mechi za nyumbani.

Mazoezi yao ya kwanza ilikuwa ni Septemba 7,2022 na mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia timu hiyo ikifanya mazoezi kwenye uwanja wao ambao kwa sasa una muonekano bora na wa kisasa zaidi.

Kinara wa utupiaji mabao ndani ya Namungo, Relliats Lusajo amesema kuwa kurejea kwao ni furaha na wataendelea kupambana kufanya vizuri.

Uwanja wa Namungo Kuanza Kutumika
Uwanja wa Namungo

“Tulikuwa nje kwa muda mrefu na tulikuwa tukitumia Uwanja wa Ilulu sasa tumerudi Uwanja wa Majaliwa hili ni jambo la kubwa kwetu.

“Haina maana kwamba Uwanja wa Ilulu haikuwa nyumbani hapana kuna kitu kinaongezeka kurejea kwenye uwanja ambao tulikuwa tukiutumia kwa muda mrefu na tunaamini kwamba mashabiki watazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Lusajo.

.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa