Fede Valverde: Nafurahia Ninachokiona Barcelona

Nyota wa Real Madrid, Fede Valverde amefurahishwa na kile alichokiona kutoka Barcelona chini ya Xavi Hernandez.

Barca wameimarika sana chini ya Xavi, wakisaidiwa na wachezaji wapya kama Pierre-Emerick Aubameyang, Ferran Torres na Adama Traore, ambao walinunuliwa kwenye dirisha la majira ya baridi.

Mabadiliko chini ya Xavi yalianza taratibu baada ya meneja huyu kuingia klabuni hapo. Barca wameshinda mechi sita kati ya saba zilizopita, na sasa wako katika nafasi ya tatu kabla ya pambano lao la Clasico dhidi ya Real Madrid wikendi hii.

Pia walijihakikishia tiketi ya robo fainali ya Ligi ya Europa siku ya Alhamisi, wakiwashinda Galatasaray ugenini kwenye mechi yao ya pili. Akizungumzia Barcelona, Valverde anasema;

“Wanacheza vizuri sana. Wamekuwa na mabadiliko makubwa sana. Wanacheza vizuri sana na inaonyesha wanataka kwenda kutafuta pointi kwenye mchezo. Kwetu sisi, tuna mchezo wetu, tutaenda kutafuta kitu kwanza na tuna silaha zetu.”


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe