Edwin Van Der Sar amejiuzulu nafasi yake kama mkurugenzi mkuu mtendaji wa klabu ya Ajax Amsterdam mapema leo na hii imetokea baada ya gwiji huyo kuitumikia klabu hiyo kwa miaka takribani kumi na moja.
Van Der Sar ametangaza kuondoka ndani ya Ajax ambapo amewahi kuitumikia klabu hiyo kama mchezaji kabla ya kua kiongozi ndani ya timu hiyo alianza kama mkuu wa kitengo cha masoko na mwaka 2016 ndio mtendaji mpaka mwaka 2023 ambapo ndio ametangaza kuachana na timu hiyo.
Gwiji huyo wa zamani wa klabu ya Ajax, Juventus, Fulham na Manchester United ameushukuru Uongozi wa Ajax, mashabiki, wachezaji, pamoja watu wote alioshirikiana nao kwa kipindi chote alichokua anaitumikia klabu hiyo kwenye kipindi cha mafanikio na kisicho na mafanikio pia.
Gwiji Van Der Sar amekua kwenye uongozi ndani ya klabu ya Ajax kwa miaka kumi na moja moja ya taasisi bora kabisa ya soka duniani, Hivo kutokana na uzoefu ambao ameupata gwiji ni wazi anaweza kufanya kazi kwenye klabu yeyote kubwa duniani.
Taarifa mbalimbali zinaeleza kua Van Der Sar ana uwezekano mkubwa wa kuungana na raia mwenzake wa Uholanzi kocha Erik Ten Hag ndani ya klabu ya Manchester United ambaye walikua wanafanya kazi pamoja, Ikiwa wakati huu klabu ya Manchester United inataka kufanya mabadiliko mbalimbali ndani ya timu hiyo.

